Matukio
BARAZA LA WAFANYAKAZI- ICoT
- 18th Sep, 2026
- Tukuyu, Mbeya Tanzania
- 11:30AM
BARAZA LA WAFANYAKAZI- ICoT
Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala wizara ya ujenzi Karim Mkorehe amesema watumishi wa taasisi ya teknolojia ya ujenzi (Icot) wana haki ya kuwa na mazingira mazuri ya kazi ,kusikilizwa,kuheshimiwaa na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za utumishi wa umma Stahiki zao
na kuwa watekelezaji wa majukumu wanayopewa
Mkorehe ambae alimwakilisha katibu mkuu wa wizara hiyo amezungumza hayo wakati wa kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa taasisi ya teknolojia ya ujenzi (ICoT) unaoendelea kwa siku mbili wilaya ya tukuyu mkoani Mbeya.
Amewataka kila mtuimishi kuendelea kufanya kazi kwa bidi na uadilifu mkubwa,kuheshimu muda wa kaz, kutunza mali za serikali na kuzingatia sheria kanuni na taratibu ikiwa pamoja na kuwahudumia wanafunzi na wadau kwa weledi.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa taasisi hiyo Mhandisi Paulo Nyanga akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli zinaazofanywa na tasisi hiyo amesema wataendelea kusimamia uwajibikaji,nidhamu na kujipang katika kukabilian na mvua za elinino kwa kutoa vifaa na Mawazo ya kitaaluma yatakayowezesha kukabili uharibifu wa mazingira unaoweza kutokea .
