HISTORIA YA ICoT
Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) imeanzishwa na Wizara ya Ujenzi ambayo iliunganisha Chuo cha Ujenzi Morogoro (Morogoro Works Training Institute – MWTI) na Taasisi ya Teknolojia Stahiki ya Nguvukazi Mbeya (Appropriate Technology Training Institute – ATTI) na kuanzisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT). Taasisi hii ina usajili wa kudumu kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa nambari ya usajili REG/SAT/035 wa tarehe 8 Februari, 2021 na inaendelea kutoa mafunzo kwa ngazi ya Astashahada (NVA daraja I hadi III) na Stashahada (NTA daraja 4 hadi 6) katika fani za uhandisi ujenzi, umeme na mitambo. Taasisi hii pia inatoa mafunzo mbalimbali ya muda mfupi kama vile mafunzo ya ujenzi wa Barabara kupitia Teknolojia Stahiki ya Nguvukazi (Labour Based Tecknology – LBT) na kozi nyingine za muda mfupi. Vilevile, Taasisi hii inajihusisha na kufanya Tafiti katika teknolojia mbalimbali katika sekta ya ujenzi na kutoa Ushauri Elekezi.
