MAFUNZO YA KOZI YA UKARABATI NA MATENGENEZO YA BARABARA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA STAHIKI YA NGUVU KAZI (LABOUR BASED TECHNOLOGY)
28th Feb, 2026
Tukuyu, Mbeya
08:00 AM
MAFUNZO YA KOZI YA UKARABATI NA MATENGENEZO YA BARABARA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA STAHIKI YA NGUVU KAZI
Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi- ICoT imeendesha mafunzo ya Kozi ya ukarabati na Matengenezo ya Barabara za udongo na changarawe kwa Makundi maalum ya wanawake, vijana, wazee na wenye ulemavu katika tawi la ICoT Mbeya.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa wiki nne (4) kuanzia tarehe 02/02/2026 hadi 28/02/2026.
Mafunzo yamefanyika kwa awamu mbili; awamu ya kwanza ilikuwa ni nadharia na awamu ya pili ikiwa ni mafunzo kwa vitendo (site).
Washiriki wa mafunzo wamepata wasaa wa kusoma masomo Kama vifaa na mitambo, vipimo vya kiufundi (technical specification), usanifu wa barabara (road construction standards), upimaji wa barabara, ukarabati wa barabara, utunzaji wa barabara, teknolojia ya usingizi, usimamiaji wa mikataba, taratibu za tenda pamoja na usimamiaji wa kazi site.