Matukio

Mahafali ya Tatu ya Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi

  • 25th Oct, 2025
  • Morogoro
  • 09:00AM - 03:00PM

ICOT KUBORESHA MITAALA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA

Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) imetangaza mpango wa kuboresha mitaala yake ili iendane na mabadiliko ya kasi ya sayansi na teknolojia. Hatua inayolenga kuongeza ushindani wa wahitimu katika soko la ajira la ndani na kimataifa.

Hayo yamebainishwa mkoani Morogoro wakati wa Mahafali ya Tatu ya ICOT, ambapo uongozi wa ICoT umeeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyofikiwa, bado wanakumbana na changamoto ya upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, hali hii inachelewesha ubunifu na ufanisi katika utoaji wa elimu.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Karim Mkorehe alisema Wizara imejipanga kuhakikisha changamoto zote zinatafutiwa ufumbuzi wa haraka.

Aidha, aliutaka uongozi wa ICoT kutatua changamoto zilizo ndani ya uwezo wao ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Mahafali hayo yaliyofanyika tarehe 25 Novemba 2025 yalishuhudia jumla ya wahutimu 63 wakikabidhiwa vyeti katika fani mbali mbali za ujenzi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuandaa wataalamu waliobobea katika sekta Muhimu za ujenzi.